Majambazi waliliteka gari moja lililokua limesheheni abiria. Baada ya abiria kusachiwa na majambazi hao na kukutwa hawana pesa, majambazi wakasema kila mtu atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa, aliyekua hana namba atasalimika

Kazi ikaanza, jamaa alievaa jezi ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pembeni kulikua na jamaa analia sana yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke simu chaji kwanza.

#ChekanaZephiline