Mwanamke Mwenye Maumbile ya Kushangaza, Ambapo Wazungu Walimtumia Kama Sehemu ya Maonyesho.
Sarah Baartman alizaliwa mnamo mwaka 1780, huko kusini mwa bara la Afrika. Jina lake la asili ni Saartie au Ssehura ambao kwa mujibu wa lugha ya Kikhosa ilimaanisha mtu mwenye umbile kubwa na la ajabu. Vyanzo vya historia vinamatambua Sarah kwamba, alitokea kwenye kabila la Wafugaji wa Khoikhoi ambao wanapatikana mashariki mwa mji wa Cape Town huko Afrika Kusini.
Sarah Baartman alikuwa na urefu wa futi 4 na nchi 7. Maisha ya Sarah akiwa huko kijiji kwao yalikuwa magumu sana kutokana na hali ya maisha ya familia yake na maisha ya kusini mwa bara la Afrika kwa miaka hiyo ya 1700.
Ambapo mama mazazi na Sarah alifariki wakati Sarah akiwa na umri wa miaka miwili tu. Inapata kusimuliwa kuwa, kabila la Khoikhoi linasifika kwa kuwa na wananawake wenye maumbile makubwa ambayo kwa miaka mingi wageni wengi walikuwa wakishangazwa na maumbile hayo. Lakini kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Khoikoi, mwanamke kuwa na maumbile makubwa ni alama ya uzuri kwa mwanadamu hususani kwa mwanamke.
Ikumbukwe tu kwamba, kuanzia miaka ya 1600, tayari maeneo ya Afrika Kusini kulishavamiwa na wageni kutoka Ulaya, yaani Wadachi na Waingereza. Na hivyo kulikuwa na maendeleo makubwa ya shughuri za kilimo. Ambapo kutokana na hali ya maisha ya Sarah, ilimlazimu kuanza kufanya kazi kama mtumwa kwenye mashamba ya wageni huko kusini mwa Afrika.
Ambapo kuna kipindi alitokea bwana mmoja wa Kidachi alimnunua Sarah kutoka kwa mwajiri wake wa shamba, na kumchukua na kumpeleka kufanya kazi za ndani. Na wakati ambao Sarah anafanya kazi za ndani, ndio kipindi ambacho watu wengi walimuona Sarah akiwa na maumbile makubwa na kilichowaangaza ni kuwa na makalio makubwa.
Unaambiwa hivi, ukubwa wa maumbile yake yalitokana na kuwepo kwa mafuta mengi kwenye misuli iliyojishikiza kwenye, kitu ambacho kiliwashangaza watu wengi waliofika na kumshangaa. Kwa mujibu wa watalamu wa masuala ya binadamu yaani Baiolojia walieleza ya kwamba, maumbile makubwa ya Sarah, ni moja ya urembo kwa jamii ya Wakhokhoi wanaoishi huko kusini mwa Afrika.
Ambapo ukiachilia mbali jamii ya Wakhokhoi, bado kuna baadhi ya jamii zingine za kibantu, wana maumbile makubwa na ya kushangaza. Mfano mzuri ni jamii ya Waonge kutoka kisiwa cha Andaman, lakini pia hata maeneo ya afrika mashariki, kwa jamii za Waganda pia kunapatikana watu wa aina ya Sarah.
Kwa Waafrika kuwa na maumbile makubwa ni suala la kawaida, lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, yaani karne ya 19, Wageni kutoka Ulaya walikuwa na mtazamo tofauti ambao ulikuwa na athari kubwa sana kwa Sarah Baartman na Waafrika kwa ujumla. Na kwamba walimuona Sarah kuwa ni mwanadamu wa kipekee na kuanza kumtumia kwa aajili ya kufanya maonyesho ya makalio yake.
Inasimuliwa kuwa, kulitokea bwana mmoja Dunlop aliyekuwa anafanya kazi kwenye meli za kivita, alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kumtumia Sarah akiwa kama mtumwa wake lakini pia alikuwa akimtumia Sarah kwa masuala ya ngono.
Ambapo kwenye miaka ya 1810, Bwana Dunlop akishirikiana na wenzake walimshamwishi Bwana Hendik Cesars kumchukua Sarah na kumpeleka mjini London nchini Uingereza na huko ndipo alipopata jina la Sarah.
Bwana Dunlop akishirikiana na Bwana Cesars walimshawishi Sarah na kumwambia kuwa, endapo mwili wake utatumika kwenye maonyesho, atapata utajiri mkubwa sana na kuja kuwa mtu maarufu hapa duniani. Ambapo bila kupinga, Sarah alikubali mwili wake utumike kwa ajili ya maonyesho.
Na mara baada ya Sarah kukubali, Bwana Dunlop akiwa na wenzake walianza kutoka matangazo nchi nzima juu ya maonyesho hayo. Na ukweli ni kwamba, maonyesho mengi yalipatwa kuhudhuriwa na watu wengi sana na moja ya nchi ambazo zilionekana kutia fola ni Uholanzi na Uingereza.
Ukweli wenye kusikitisha ni kwamba, kwa kipindi chote cha maonyesho, Sarah alikuwa akitunzwa kama mnyama wa maonyesho. Na kwamba maisha yake alikuwa hatofautiani na wanyama wengine wafugwao.
Na kipindi chote cha maonyesho Wanaume na wanawake walikuwa wanapata nafasi ya kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake. Na wengi walionekana kufurahia jambo hilo. Wengine walidiriki kumtupia vyakula kama anavyotupiwa nyani au kima.
Kwa wakati wote huo wa maonyesho, walitokea baadhi ya wanasayansi yaani Madaktari ambao walikuwa na mitazamo tofauti tofauti. Wapo waliodai kuwa, muonekano huo wa Sarah ni ugonjwa wa Macronymphy ambao ameupata na unapatikana huko Afrika. Kitu ambacho hakikuwa kweli na kwamba, kwa Waafrika suala la mtu kuwa na maumbile makubwa ni suala la Kawaida tu.
Kuliwahi kutokea mwanaharakati mmoja kutoka huko Jamaika aliyeitwa Robert Wedderburn, huyu ndio mtu pekee aliyejitokeza kwa ajili ya kumpigania Sarah. Na mara kwa mara alitumia muda wake kuishinikiza serikali ya Uingereza kuacha mara moja unyanyasa kwa watu weusi. Ambapo kwake yeye aliona jambo hilo ni kama Utumwa.
Mwaka 1814, Bwana Denlop pamoja na mshirika wake bwana Cesars waliamua kumuhamisha Sarah na kumpelekea mjini London. Na hii ni kutokana na harakati za bwana Robert Wedderburn. Ambapo akiwa huko Ufaransa Sarah alioneshwa kwenye kumbi mbalimbali huko mjini Paris ambapo huko napo alipewa majina mbalimbali kutokana na maumbile hayo.
Inapata kusimuliwa kuwa, akiwa huko mjini Paris, Sarah alikuwa akitumika kama chombo cha ngono, ambapo aligeuzwa na kuwa kama mwanamke anayejiuza yaani "Malaya". Na mara nyingi alikuwa akifanyiwa vitendo vya ngono adharani huku mamia ya watu walitazama wake kwa waume.
Alitokea Bwana mmoja huko mjini Paris aliyefahamika kwa jina la Georges Cuvier, ambaye alikuwa Daktari wa Napoleon Bonaparte, ambaye pia alikuwa mkurugenzia wa French Natural Museum Natural History. Ni mtu pekee nchini Ufaransa aliyepata nafasi kubwa ya kumfanyia Sarah utafiti na kutoa ripoti za kishenzi kadiri alivyotaka.
Sarah Baartman alifariki akiwa na miaka 26 huko mjini Paris mnamo tarehe 29/12/1815. Kifo chake kilitokana na kuumwa ugonjwa wa Homa ya Mapafu yaani Pneumonia, kutokana na mwili wake kutumika kwa muda mrefu na mtindo wa maisha yake kwa ujumla.
Ambapo kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa waataalamu wa afya, walisema kuwa, kifo chake kimesababishwana matumizi mengi ya pombe kali, alizokuwa akitumia wakati wote wa maonyesho. Kutokana na kifo cha Sarah, baadhi ya ripoti mbaya kuhusu Waafrika ziliandikwa, na kwamba Waafrika ni watu dhaifu sana kwani Sarah alifariki akiwa na mdogo sana.
Miaka ya baadae yaani mwaka 1975, huko nchini Ufaransa, kulifanyika maonyesho ya baadhi ya mabaki ya mwili wa Sarah. Na mpaka kufikia mwaka 1994, Nelson Mandela, alichaguliwa kuwa raisi wa Afrika Kusini, ambapo aliomba serikali ya Ufaransa kurudisha mabaki ya mwili wa Sarah, ambayo ni mali ya serikali ya Afrika Kusini.
Mwanzoni serikali ya Ufaransa ilipuuzia maombi hayo, lakini mnamo mwaka 2002, serikali ya Ufaransa ilikubali kurudisha mabaki hayo. Na mara baada ya mabaki hayo kufika huko Afrika Kusini, yalizikwa sehemu ambayo Sarah alipozaliwa, na hii ni baada ya miaka 192 tangu aondoke katika ardhi ya Afrika Kusini.
Na ili kutunza historia ya Sarah Baartman kuliandikwa vitabu vingi sana, kulitengenezwa filamu kadha wa kadha kama ile ya "Black Venus" ya mwaka 2010, kulitengenezwa Makala ya Video iliyojulikana kama "The Life and the Times of Sara Baartman" ya mwaka 1998.
Inasimuliwa kuwa, pamoja na Sarah kufahamika na watu wengi, bado kuna taarifa nyingi sana kuhusu Sarah ambazo hazifahamiki. Je? unafahamu jambo gani kuhusu Sarah Baartman? Usiache kuandika maoni yako hapa. Ahsante
#CnZHistoria