Ndege ilipata hitilafu angani Rubani akatoa taarifa kwamba ndege imepata hitilafu na itadondoka baada ya dakika 10, ndani ya ndege kulikuwa na watu watano lakini parashuti zilikuwa nne tu

Watu hao ni Mchungaji, Waziri, Mwanajeshi, Msukuma na Mwanafunzi wa chekechea, Mchungaji akasema yeye anategemewa na kanisa hivyo hapaswi kufa hivyo akachukua parachuti akaruka, Waziri akasema wananchi wanamtegemea alete maendeleo, akachukua parachuti akaruka, Msukuma akasema familia inamtegamea akachukua parachuti akaruka haraka, wakabaki Mwanajeshi na Mwanafunzi wa chekechea

Yule Mjeshi akamtazama Mwanafunzi akamuonea huruma kisha akasema "Mimi najitolea kufa kwa ajili yako, we chukua hilo parachuti lililobaki ujiokoe halafu mimi nitakufa na hii ndege" yule Mwanafunzi akajibu "Usijali yamebaki maparashuti mawili" yule mjeshi akashangaa akauliza "Mawili kivipi!?" Mwanafunzi akasema "Yule Msukuma kachukua begi langu la shule akidhani ni parachuiti"

#ChekanaZephiline