Zifahamu dalili za awali na za mwisho za ugonjwa wa UKIMWI 00018
Habari za muda huu mpenzi msomaji wa Muungwana Blog bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nikukaribishe ili uweze kujifunza dalili za awali na za mwisho ambazo huonekana kwa mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Zipo dalili za awali ambazo huonekana kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi.

Dalili hizo awali ni kama ifuatavyo;


  1. Homa
  2. Kusikia baridi
  3. Maumivu ya joints
  4. Maumivu ya misuli
  5. Koo kavu
  6. Jasho (Hasa usiku)
  7. Uchovu wa mwili
  8. Udhaifu
  9. Kukonda


Baada ya dalili hizi za awali kutoweka, mara nyingi hakuna dalili zo zote zitakazooneka kwa kipindi kirefu. Wakati huu wadudu hawa wanazidi kuzaliana, kuongezeka na kuharibu mfumo wa kinga za mwili. Kipindi hiki cha ukimya kinaweza kwenda hadi miaka 3 wakati huu wote mtu akijisikia vizuri tu na kuonekana mwenye afya.

Na ndio maana mara nyingi watu hushauriwa kupima virusi vya ukimwi kila baada ya mwezi ili kujua kama atakuwa ameambukizwa.
Baada ya kuona dalili za awali sasa naomba tuangalie dalili mwisho za ugonjwa huu.

Dalili za mwisho za UKIMWI zinaweza kuwa:


  • Kutoona vizuri.
  • Kuharisha mfululizo.
  • Kikohozi kikavu.
  • Homa kali inayokwenda kwa muda mrefu.
  • Kuvuja jasho usiku.
  • Uchovu wa mwili mfululizo.
  • Kupumua kwa shida.
  • Kukonda.
  • Vijidoa vyeupe kwende midomo na ulimi.


Hivyo kila wakati hakikisha unakwenda kwenye vituo vya afya ili Kupata ushauri lakini pia  kupima kama una mambukizi ya virusi vyaUKIMWI.