China Kutengeneza Kituo cha Anga Chakwao(CNSA) 15994410
China National Space Administration (CNSA) wapo mbioni kurusha vipande ambavyo vitaenda kuungana angani na kuform Space Station ambayo itakuwa inamilikiwa na wachina wenyewe . China inajenga hii Station bila ya kuwa na washirika wowote ila itakaribisha mawakala watakao taka kujiunga nao...

Hatua ya China kutengeneza kituo cha anga chao inakuja baada ya kuzuiliwa na marekani na kuamliwa kutoa kituo chao katika ISS baada ya kugundulika kuwa alikuwa akiiba data kutoka kwa wanasayansi wa NASA katika chuo cha California kitengo cha Jet Propulsion ambao ni watengenezaji na waratibu wakubwa wa mission zisizobeba watu.... sababu nyengine China alikuwa akitumia satellite kama siraha ya kuwaangamiza wengine.
China Kutengeneza Kituo cha Anga Chakwao(CNSA) 7b725010
Chombo hicho cha China kitakachokuwa na uzito upatao 66 Tons kitakuwa na uwezo wa kubeba wanasayansi 4-7 ambao watafanya kazi humo ndani...

Chombo hicho kitajumuisha sehemu ya malazi na kuishi na mjumuisho wa mahitaji yote ya mwanadamu na pia kitakuwa na upande wa maabara ya kufanyia vipimo vya kisayansi...

Kituo hicho kitarushwa angani kwa awamu 7 mpaka kukamilika na kitarushwa na rocket kubwa ya Long March 5b na pia kitachukua takribani miaka 2 na nusu mpaka kukamilika

Mkurugenzi wa shirika la anga la china amesema hawato wabagua watu kama wafanyavyo wamarekani kwamba uwezi kuwa mwanasaynsi wa NASA mpaka upitie jeshini au uwe ulishawahi kuwa rubani, China wao watachukuwa wale wote wanayoiweza sayansi haswa ya Physics

China Kutengeneza Kituo cha Anga Chakwao(CNSA) 49176210
Pia China wako mbioni kurusha Telescope yao iitwayo XUNTIAN Telescope ambapo itakuwa na uwezo sawa na Hubble Space Telescope ya Marekani

Kutengenezwa kwa station hii kutaongeza wakuu wawili kwenye mambo ya anga

Wanasayansi wetu wa Tanzania wajitahiji watengeneze na wao sehemu ili twende tukaunganishe na station ya wachina maana wachina ni marafiki zetu

Nini maoni yako? Weka comment yako hapa