RAFIKI YANGU ANATAKA KUTEMBEA NA MUME WANGU WAKATI WOTE TUMEAMBUKIZWA 0000012
RAFIKI YANGU ANATAKA KUTEMBEA NA MUME WANGU WAKATI WOTE TUMEAMBUKIZWA JE NIMUAMBIE AU NIMUACHE?

Mimi ni mwanamke wa miaka 37, nimeolewa na Mungu kanijaalia watoto watatu. Mimi na mume wangu wote tunaishi na virusi vya ukimwi, mwaka watatu sasa tangu nigunude ila mume wangu anaonekana alishajua muda mrefu kuwa kaathirika lakini akanifanyia makusudi. Nistori ndefu lakini ni kama nilijitakia kwani mwanaume wangu ni Malaya sana na nilikua nikivumilia mpaka aliponiambukiza.

Sababu ya kuomba ushauri nikuwa, nimefumania meseji za mapenzi kati ya mume wangu na rafiki yangu mkubwa. Niyule rafiki wa karibu sana najua kila kitu kuhusu yeye na yeye anajua kila kitu kuhusu mimi. Mume wangu kamtongoza naona kama kaingia laini na amemkubali, wamepanga kesho kwenda nnje ya mji, mume wangu kashaniaga kabisa anasafari ya kikazi na rafiki yangu kanidanganya anaenda kwa Mchumba wake ambaye haishi hapa.
Sasa hapa nawaza je nimuambie rafiki yangu kuhusu hali ya mume wangu ili asijeuvaa mkenge au nimuache aendelee kunisaliti aambukizwe ili tunywe ARV pamoja? Niko njia panda sijui nifanye nini? Kinachoniumiza zaidi nikuwa huyo rafiki yangu ni mjamzito na kusema ukweli ana mwanaume ambaye anampenda sana. Sijui ni kitui gani kimemkuta lakini ana ile aina ya wamaume ambao ukimuona unatamani. 

Huyo Kaka anafanya kazi, kipato chake ni cha kawaida tu lakini anamhudumia kwa kila kitu, anajitoa na wanafamua mambo ya maendeleo kwa pamoja. Ameshajitambulisha kwao na mipango ni kufunga ndoa mwezi wa nne mwaka huu. Hapa nawaza nifanye nini, mume wangu ni wale wanaume ambao wana hasira na nahisi aligundua kuwa ameambukizwa muda mrefu na alikua anafanya mapenzi na wanawake wengi ili kuwaambukiza. Hata mimi nilivyomuuliza kwanini alijua muda mrefu kuwa kaambukizwa na bado akaniambukiza alinijibu vibaya.