Miongoni mwa magonjwa ambayo husumbua watu wengi kwa kiwango kikubwa ni moyo, hivyo ili kuweza kulinda afya ya moyo wako ili usipate magonjwa hayo ya moyo unatakiwa kufanya yafuatayo;
- Pima shinikizo la damu angalau mara moja kwa mwaka.
- Hakikisha unakuwa na uzito sahihi.
- Fanya mazoezi walau nusu saa kwa siku.
- Punguza matumizi ya chumvi kwenye chakula. Hapa tunanzungumzia chumvi ya mezani ambayo huongezwa kwenye vyakula kama vile nyama choma, chipsi n.k
- Kila wakati hakikisha unakula zaidi matunda,mboga za majani na vyakula ambavyo havina mafuta.
- Punguza matumizi na unjwaji wa pombe.
- Iwapo umegundulika kuwa na tatizo la shinikizo la damu,tumia dawa kama ulivyoelekezwa na watalamubwa afya na si vinginevyo.