Faida zitokanazo na tunda la Stafeli kiafya 00015
Tunda hili lenye rangi ya kijani hata likiwiva, lina virutubisho vingi ikiwamo asidi ya amino, vitamini C, madini ya chuma, phosphorus, calcium, carbohydrate na nyuzinyuzi zinazohitajika wakati wa tendo la usanisi wa chakula tumboni.

Utafiti uliofanywa miaka ya hivi karibu katika Chuo Kikuu cha Purdue, Marekani, ulibaini uwezo mkubwa wa mstafeli katika kukabiliana na maradhi ya saratani.

Chuo hiki kinachojihusisha na masuala ya dawa, kilibaini kuwa licha ya mizizi, majani na tunda kuwa ni msaada kwa wanaokabiliwa na saratani pia stafeli linasaidia wale wanaokabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo na mfadhaiko.

Licha ya kuwa suala la stafeli kutibu saratani linaweza kuzua mjadala, lakini hakuna shaka kwa kuwa lina virutubisho vingi yenye uwezo wa kupambana na makali ya maradhi hayo.

Ukweli huu unawapa wagonjwa wa saratani njia pana zaidi ya kukabiliana na maradhi haya kwani pamoja na tiba nyingine, stafeli lina nguvu ya kupunguza makali au kuwapa kinga licha ya kuwa wanatumia mionzi .
Habari njema ni kwamba mmea huu ambao naweza kuuita ni wa ajabu kutokana na nguvu yake  katika tiba, unapatikana nchi nzima kwa maana ya mijini na vijijini.

Zaidi ya majaribio 20 ya kimaabara yaliyofanywa kuhusu uwezo wa stafeli yamebaini kuwa huua chembechembe za aina 12 za saratani ikiwamo ya titi, mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.

Tafiti hizo zimefafanua kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu saratani na magonjwa mengine kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida.

Mchanganyiko wa virutubisho vya annonaceous na acetonins vilivyomo kwenye stafeli vinaua seli zilizo athirika na saratani tu tofauti na dawa za kisasa ambazo zinaua zilizoathirika na nzima.

Stafeli linadhibiti ukuaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine kama ilivyo kwa dawa za kisasa zina athari mbaya kwa mtumiaji na wakati mwingine zinaweza kumsababishia matatizo mengine ya kiafya.

Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Uingereza (NIR), ilibaini kuwa mstafeli ni tiba ya saratani kuanzia mizizi, majani na hata tunda lake.

Pamoja na utafiti huo kufanyika mwaka 1976 bado haukuwekwa wazi kwa sababu za maslahi ya kibiashara.