Cheka na Zephiline
Ingia(Log In) Kwenye Akaunti Yako
Kama Hauna Akaunti
Jisajili(Register)
Ili Ufurahie Kuchat/Kuchekeshana na Wenzako na Kusoma Simulizi


Cheka na Zephiline
Ingia(Log In) Kwenye Akaunti Yako
Kama Hauna Akaunti
Jisajili(Register)
Ili Ufurahie Kuchat/Kuchekeshana na Wenzako na Kusoma Simulizi

Cheka na ZephilineLog in

Tucheke na Kufurahi Pamoja na Kubadilishana Mawazo #ChekanaZephiline

Kama unapata shida ya kujiunga njoo WhatsApp +255 718274413 nikupe msaada
Kama unapata shida ya kutumia forum yetu njoo PM Box(inbox) nikupe usaidizi

Karibuni Sana Tucheke na Kuenjoy Kila Siku
#ChekanaZephiline

'I Can't Share my Man'

Ulipokuwa Single Ulikuwa Bingwa wa Kuiba Waume za Watu Bila Uoga, Leo Umeolewa Unasema "I CAN'T SHARE MY MAN", Vaa Upesi Ukakanyage Mafuta kwa Mwamposa

#ChekanaZephiline

Vodacom Wanatoa Ofa

BREAKING NEWS
'Vocodam inatoa 2GB Kama zawadi' hivi ndivyo ulivyofeli mtihani, umeona wapi pameandikwa Vodacom?

#ChekanaZephiline

NAMNA YA KUJUA KAMA MTU WAKO ANA MCHEPUKO

Soma na fuata masharti vizuri:

1. Chukua simu yake kisha pata namba yake ya IMEI, kwa kuminya *#06#, kisha andika namba hiyo pembeni.
2. Chukua namba ya IMEI yako na namba ya vocha uliyotumia mara ya mwisho, andika pembeni.
3. Subiri mpaka dakika chache kabla ya saa sita usiku maana huu ndio muda kompyuta zinabadili tarehe. Kisha kwenye simu yako andika meseji hii *00002020*165239* kisha weka IMEI namba yako * IMEI ya mpenzi wako *, namba ya vocha uliyohifadhi#, tuma meseji kwenye namba 7567563314.
4. Itakuja namba ambayo baadae utaituma kama vile unataka kuongeza fedha kwenye akaunti yako, itume kwenye simu ya mpenzi wako.
5. Kisha kwenye simu yako ingiza namba 65231 piga itakufikisha kwenye inbox ya mpenzi wako. Kilichobaki sasa ni pass word ya kufugua inbox hiyo. #MUHIMU
6. Ikiwa bado unafuatilia kwa makini maelezo haya magumu na ya kipuuzi /kijinga Ina maana humuamini mpenzi wako. Sasa kwanini usiamtafute mpenzi mwingine kabla hujafa kwa presha.

#ChekanaZephiline

Msalimie Njaa

Felister: Mambo mpenzi
Mimi: Poa tu bby
Felista: Niko hapa town honey,,,,
Mimi: Oooh that Nice
Felister: Niko na njaa hapa Honey
Mimi: Oooh msalimie sana

#ChekanaZephiline

Mbinu Mpya ya Wazazi

Wazazi wamegundua jinsi ya kukwepa bili za zawadi kwenye harusi za watoto wao, halafu ni kama wapo group moja WhatsApp au Telegram wana share idea
"Tunawapatia kitu cha thamani kubwa kuliko vyote duniani, kitabu hiki cha dini kitawaongoza na kuwapa yote mtakayo, tunawapenda sana"

#ChekanaZephiline

Yupo Kwenye Siku Zake

Nimejiandaa na Al-Qasuus, Vumbi la Congo, Mundende pamoja na K-Vant halafu demu ananiambia yupo kwenye siku zake, nitamalizia wapi haja zangu!?

#ChekanaZephiline

Ua na Boga

Ukipenda mke wa mtu penda na mume wake

#ChekanaZephiline

Kuna B Ngapi?

Heu jaribu kutumia uwezo wa macho yako kama yanaona vizuri. Kuna herufi B ngapi hapo? 88888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888B88888888888B888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888B888888888888888888888888888888888888888888888B88888888888888888888888888888B88888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888B888888888888

#ChekanaZephiline

Baba Mzazi Anachepuka

Ukimuona Baba yako mzazi anakisiana na mwanamke mwingine njiani utafanyaje?
1. Utapita kimya kimya
2. Utakohoa
3. Utamsuta Baba yako
4. Utaenda kumwambia mama yako

#ChekanaZephiline

Jengeni Kama Mimi

Mary: Mambo?
Ally: Poa
Mary: Mbona kimya?
Ally: Nipo
Mary: Baby nadaiwa kodi ya nyumba hapa
Ally: Mi nilizijua hizo kero ndio maana tukajenga nyumba na mke Wangu
Mary: What.?
Ally: Nyumba
Mary: Umenichoka kwa Kweli
Ally: Tafuta mwanaume mwenye akili kama mimi mjenge

😂🤣😂🤣😂🤣
#ChekanaZephiline

Mwanaume Anayenukia Vizuri

Hakuna mtu anayenukiaga vizuri kama yule unayempenda, ila mkishagombana tu sijui harufu ya beberu hutokeaga wapi?😂🤣

#ChekanaZephiline

Mfupi Ndio Mkorofi

Ukikuta wadada wawili wanatukanana jua yule mfupi ndio mkorofi😂🤣

#ChekanaZephiline

Kitovu cha Mwanaume

Mwanaume kuwa na kitovu kilichodumbukia ndani huo ni UMAMA
Kitovu cha mwanaume inabidi kitokeze nje kama tonge la ugali😂🤣

#ChekanaZephiline

Kifo ni Nini?

KIFO NI NINI?
Kifo ni pale unapokosea text ukamtumia baba yako 'Hellow Mrembo' wakati mnakula😂🤣

#ChekanaZephiline

Simu ni Simu

'Simu ni simu tu ilimradi kuna WhatsApp, Instagram na Facebook'
Hivi ndio jinsi watumiaji wa Tecno, Infix na Itel wanavyofarijiana

#ChekanaZephiline

Valentine Day

Kipindi hiki kuelekea msimu wa Valentine wanawake wanajifanya romantic na kuomba msamaha hata vitu ambavyo haviwahusu, utasikia 'Baby naomba unisamehe mimi kwa Simba kufungwa magoli matano'😂🤣

#ChekanaZephiline

February Yenyewe Kipisi

Hauwezi zaliwa February ukawa Mzima wakati mwezi wenyewe haujakamilika😂🤣

#ChekanaZephiline

LOWASA 2015

Majambazi waliliteka gari moja lililokua limesheheni abiria. Baada ya abiria kusachiwa na majambazi hao na kukutwa hawana pesa, majambazi wakasema kila mtu atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa, aliyekua hana namba atasalimika

Kazi ikaanza, jamaa alievaa jezi ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pembeni kulikua na jamaa analia sana yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke simu chaji kwanza.

#ChekanaZephiline

Ipi Kauli ya Mama Inaboa?

Ukiachana na 'Nikirudi nikute vyombo vimeoshwa' ni kauli gani nyingine ya Mama yako huwa/ilikuwa inakuboa?

#ChekanaZephiline

Nataka EX Wangu Aumie

Jamani mwenye picha na video za maneno mazuri mazuri huko ulaya anitumie chaaap, EX wangu yupo online muda huu anatazama post zangu, nataka ajue nimeshahama nchi😂🤣

#ChekanaZephiline

Wanawake Bila Filter Hawanogi

Yaani wanawake siku hizi ni kama SIGARA bila FILTER hawanogi😂🤣

#ChekanaZephiline

Msimu wa Sikukuu Ukikaribia

Ukiona demu wako kazidisha kukuita Baby, Honey, Sweetheart, Love, Hubby etc. ujue msimu wa sikukuu umekaribia

#ChekanaZephiline

Ikawe Wiki ya Mafanikio

Ikawe wiki ya Mafanikio kwenu sote, Mungu atusimamie na tutimize malengo
#Amina #Amen

#ChekanaZephiline

Mwanamke Kata Viuno

Katika maisha mwanamke haupaswi kukata tamaa, unatakiwa ukate viuno tu mpaka mwanaume apatwe na tamaa ya kukuoa

#ChekanaZephiline

Adam Alifeli Wapi?

Hivi ni kwanini Adam hakukataa kula Tunda?
Alikuwa na matatizo gani?

#ChekanaZephiline

Kushangaa Wowowo

Ukiachana namimi nani mwingine huwa anavuka Barabara kwenda tu kushangaa mdada mwenye wowowo?😂🤣

#ChekanaZephiline

Nimekula Hasara

Hivi ukila hasara inatakiwa ushushie na nini?
Hapa nilipo nimekula hasara ndugu zangu

#ChekanaZephiline

Nimekula Hasara

Hivi ukila hasara inatakiwa ushushie na nini?
Hapa nilipo nimekula hasara ndugu zangu

#ChekanaZephiline

Mwenye Bikra

BAADA ya TENDO
Salha: Baby una mawazo gani na kesho yako?
Zephiline: Nataka kuoa mwanamke Bikra...

#ChekanaZephiline

Urembo sio Tabia

Ogopa sana mwanamke anayezani urembo wake ni bora kuliko tabia yake
Kama unaye kaa naye mbali huyo ni mchawi

#ChekanaZephiline

Mti wa Baba

Wakati nipo darasani nafundisha darasa la kwanza C nikauliza 'Taja aina mbili za Miti' mwanafunzi mmoja akasimama na kujibu 'Mti wa msituni na mti wa Baba'
Hapa nawaza kuacha kazi tu

#ChekanaZephiline

Punyeto

Leo kwenye kikao cha familia nilitaka kuchangia mara namsikia mjomba anasema "Kaa kimya hatuongelei habari za Punyeto hapa"

#ChekanaZephiline

Baby Baba Yako

Teddy: Naomba tuachane mimi nawewe, siwezi kuishi maisha kama haya na wewe, tena nimechoka
Zephiline: Kwanini jamani!!, umeshapata mwingine tena?
Teddy: Ndio na ni handsome na tajiri kuliko wewe
Zephiline: Jina lake Johnson?
Teddy: Mnh!... wewe umemjuaje?
Zephiline: Hiyo ni akaunti yangu feki facebook
Teddy: OMG...! Jamani baby am sorry...
Zephiline: Baby baba yako

#ChekanaZephiline

2011...

2011 ulikuwa unasoma darasa la ngapi?

#ChekanaZephiline

Wanyama Wangemiliki Hela

Wanyama wangekua wanamiliki hela wadada wangekua polini, utasikia "Jomoon baby Choii napenda madoa yako"

#ChekanaZephiline

Mahusiano ya Siku Hizi

Mahusiano ya siku hizi ni presha tupu, mnakaa na wasiwasi kama mnachemsha maziwa

#ChekanaZephiline

Andika Neno SAMAKI

Fumba macho kisha comment neno SAMAKI tuone uwezo wako
Usihariri wala kufuta tafadhali

#ChekanaZephiline

A+BxC=?

A+A+A=3
B+B+A=5
C+C+B=8
A+BxC=?

#ChekanaZephiline

Mtaachana Tu

Anakupigia simu eeh!, Anakutumia Text kila wakati eeh!
Relax, hata sisi tulianza hivyo hivyo mtaachana tu

#ChekanaZephiline

Safari Utajifungua Wakiume

Kuna mwanamke mjamzito alikaa vibaya mbele ya Kipala
Kipala: Naona safari hii unajifungua mtoto wa kiume
Mwanamke: Kwanini?
Kipala: Nimeona ndevu zake

#ChekanaZephiline

Wanawake Kunyonya ???? Mmefunzwa na Nani?

Wanaume kunyonya matiti tulijifunza kutoka kwa Mama zetu
Sasa nyie wanawake nani aliwafundisha kunyonya Makagali🍆?

#ChekanaZephiline

Sehemu za Siri

Sehemu za siri za mwanamke ni kavu ila mwanaume akizigusa hulainika
-Hii inatufundisha kuwa, mwanaume siku zote hufanya maisha ya mwanamke kuwa mepesi

Sehemu za siri za mwanaume ni laini lakini mara tu mwanamke anapozigusa gusa huwa ngumu wakati huo huo
-Hii inatufundisha kuwa, siku zote mwanamke hufanya maisha ya mwanaume kuwa magumu pindi wakiwa pamoja

NAOMBA TUSIBISHANE

#ChekanaZephiline

Ukitenda Jambo Unajitendea Mwenyewe

Kuna kijiji kimoja kulikuwa na mama mmoja kichaa, yule mama akawa anapita mitaani na kupiga kelele huku akisema "Ukitenda mema unajitendea mwenyewe na ukitenda mabaya, unajitendea mwenyewe"

Basi kila siku alikuwa anazunguka na kusema maneno hayo hayo, akisikia njaa anaenda nyumba yoyote anaomba chakula anakula anaendelea na safari zake kama kawaida

Kutokana na hilo, akawa amezoeana na watoto wote wa kile kijiji, siku moja mama mmoja akasema "Huyu kichaa anasumbua sana na anaharibu watoto wetu tumuuwe"

Siku iliyofuata yule kichaa na kelele zake kama kawaida akafika kwenye ile nyumba ya yule mama akaomba chakula, yule mama akachukua mikate akaweka sumu akampa, yule kichaa akaondoka zake na mikate yake mkononi, njiani akakutana na watoto wanatoka shuleni, wakaanza kumchezea kama kawaida yao yeye akawapa ile mikate wakala

Baada ya kuwapa mikate yeye akaendelea na safari zake, watoto walipofika nyumbani, wakaanza kuumwa matumbo mama yao akawauliza "Mmekula nini shuleni?" wakamjibu "Hatujala chochote ila tulikutana na 'Ukitenda Mema , Umejitendea Mwenyewe' akatupa mikate tukala", yule mama akaweka mikono kichwani akaanguka na kupoteza fahamu

Baada ya kuzinduka akakuta watoto wake wote wamepoteza maisha

UKITENDA MEMA, UNAJITENDEA MWENYEWE na UKITENDA MABAYA UNAJITENDEA MWENYEWE

#ChekanaZephiline

Kuoga na Baby

Ulishawahi kuoga na Baby wako au tuache mambo mengine yapite?

#ChekanaZephiline

Adamu na Eva

Huwa nawaza kama Adamu na Eva waling'ata tunda mara moja tu hali ipo hivi je wangekula lote tungekuwa wapi?

#ChekanaZephiline

Wanapenda Hela Sana

Dada zetu wanapenda sana Hela kuliko Ngono lakini cha ajabu wanapata sana Mimba kuliko Utajiri

#ChekanaZephiline

Kama Unatembea na Mke wa Mtu

Kama unatembea na mke wa mtu fuata maelezo yafuatayo Nguruwe wewe

1. Akikupigia simu pokea halafu subiri aanze yeye kuongea maana labda aliekupigia mumewe, Kenge wewe

2. Musizoee kuingia gesti moja kila munapokutana maana watu watawachora na kutoa taarifa, Mbwa wewe

3. Mukiingia gesti musiandikishe majina yenu halisia, Paka wewe

4. Ukimpigia simu akakata usipige tena labda yupo na mumewe, Kuku wewe

5. Usipende kumtumia SMS za kimapenzi kila mara, Bata wewe

6. Mmewe hata akisafiri usiende nyumbani kwake, Kunguni wewe

7. Mmewe hata akisafiri usimruhusu alale kwako muambie akalale kwake, Ngedere wewe

8. Kama jirani yako usimzoee sana watu watawastukia, Mjusi wewe

9. Usipende kupiga nae picha na kuposti mtandaoni, Fisi wewe

10. Mahusiano yako musimshirikishe shoga yake wala rafiki yako, Nyani wewe

11. Usitembee na mke wa mtu tafuta wa kwako, Nguchiro wewe

12. Comment na kushare ujumbe huu, Sisimizi wewe

#ChekanaZephiline

Bado Wewe

Kuna mzee kila tukikutana nae kwenye harusi ananiambia 'Kijana bado wewe' leo nimekutana nae kwenye msiba namimi nikamwambia 'Mzee bado wewe'

#ChekanaZephiline

Kibaby Chako

Umewahi kukiangalia kibaby chako kwa makini kisha kimoyomoyo ukaanza kujiuliza 'Ni nini hiki...!?'

#ChekanaZephiline

02/02/2021

Jamani ni tarehe 02/02/2021 hivyo kuweni makini hizo 2 msije kuzichanganya ya kwenye tarehe ukiiweka kwenye mwaka hali itazidi kuwa mbaya zaidi

#ChekanaZephiline